Kanda ya KusiniMajiMtwara

Wananchi na mifugo kata ya Nanguruwe wapokezana kunywa maji ya madimbwi

Ni takribani miaka miwili sasa wakazi wa kata ya Nanguruwe wilayani Mtwara wanalazimika kutumia maji ya kwenye madimbwi baada ya pumpu iliyokuwa ikitumika kusambaza maji kwenye mabomba katika vijiji vyao kuharibika. 
 
Wakazi wa kata hiyo wanasema kutokana na hali hiyo  wanalazimika kutumia maji hayo kwa kuwa hawana chanzo kingine cha maji ambapo wakati wa kiangazi hali huwa tete zaidi baada ya madimbwi hayo kukauka.
 

Mwenyekiti wa kijiji cha Nanguruwe Said Abdullahman anasema kuwa mwaka jana serikali ilichimba kisima kipya lakini mpaka sasa pampu ya kuvuta maji haijawekwa pasipo kujua tatizo ni nini 

Je ni upi mkakati wa serikali wa kurudisha huduma ya maji kwa wakazi wa Nanguruwe?

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close