Uncategorized

PEMBEJEO: uchumi wayumba baada ya wanyonge kushindwa kuzifikia kirahisi

Kahawa ni zao kuu la kiuchumi kwa wakazi wanao kadriwa kuwa  milioni mbili laki nne, elfu hamsini na nane na ishirini na watatu mkoani Kagera, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2012.

Katika miaka ya 1950 hadi 95, zao hilo liliwezesha familia laki mbili na nusu kusomesha watoto wao na kumudu mahitaji megine ya msingi kama chakula na ujenzi wa makazi bora.

Tangu mwaka 1997, uzalishaji wa zao hilo umeshuka na kuufanya mkoa kushindwa kutimiza lengo la uzalishaji wa tani elfu 68 kwa mwaka, kwasababu ya kushambuliwa na ugonjwa wa mnayauko fuzari, huku wakulima wakishindwa kupata miche bora na kukata tamaa ya kuendelea na kilimo cha kahawa.

Ni baadhi ya wakulima katika kitongoji cha Nyamugaba Mwanzo mgumu wilayani Misenyi, ambao wamekwishakata tamaa kabisa ya kulima zao hilo, akiwemo mzee Khalid Habibu mkulima wa eneo la Nyamugaba Mwanzomgumu katika halmashauri ya Misenyi, ambaye mwaka 1995 alipanda miche elfu moja na 500 aina ya korona, kwenye shamba ambalo kwasasa ni eneo la wazi likiwa limekanda baada ya kug’oa mibuni yake mwaka 2003, aliposhauriwa kuing’oa na taasisi ya utafiti wa zao la kahawa TACRI.

Mavuno ya awali tangu kupandwa kwa shamba hilo, yalikuwa ni magunia hamsini lakini kadri miaka ilivyokuwa ikipita mavuno yaliendelea kupungua na kufikia magunia 11 mwaka 2000, kabla ya kushauriwa kuing’oa mwaka 2003.

Halmashauri ya Misenyi ambayo imesalia na eneo la hekari elfu mbili za mashamba ya kahawa ambayo inatajwa kuwa ni nusu ya mashamba yaliyokuwepo kipindi kahawa ikipewa kipaumbele, uzalishaji wake umekuwa mdogo kwa mwaka 2014/15 tani 365 tofauti na lengo la tani elfu moja na 700,  mwaka 2015/16 walizalisha tani 428 na kilo 927 pekee, wakishindwa kufikia lengo la tani 1200 kwa mwaka huo, sababu kubwa ikiwa ni wakulima kukata tamaa ya kilimo hicho baada ya kahawa kushambuliwa na magonjwa, kama Tapita Tovana Solomo ambaye ni afisa kilimo umwagiliaji na ushirika wa wilaya, alivyoeleza sababu za kushindwa kuendeleza zao hilo

Takwimu za ofisi ya takwimu taifa NBS zilizotolewa mwaka 2014, zinaonesha pato la mkoa GDP ni shilingi milioni 3.5 sawa na kipato cha mkulima cha shilingi milioni moja na laki moja, na kuufanya mkoa huo kuwa katika nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya mikoa 21, kushuka kwa pato la mkoa kulitokana na uzalishaji wa kahawa kuwa tani elfu 30 pekee tofauti na tani elfu 68 zinazolengwa kuzalishwa.

Sautiyamnyonge imemtafuta Adam Mohammed Swahi ambaye ni katibu tawala msaidizi upande wa uchumi na mratibu mkuu katika sekta ya kilimo biashara na ushirika wa mkoa wa Kagera, kueleza athari za ukosefu wa miche bora ya kahawa katika uchumi wa mkoa.

Magonjwa ya mnyauko fuzari yanayoshambulia kahawa, yaliripotiwa mwaka 1997 mkoani Kagera, tangu wakati huo wakulima wa zao hilo wakaanza kupata mavuno kidogo na kusababisha waliowengi kukata tamaa, na kuisukuma taasisi ya utafiti wa zao la kahawa TACRI kuanza kufanya utafiti wa miche bora mwaka 2004, kwa kutumia sampuri 175 za miche 875 zilizoambukizwa ugonjwa kwa majaribio katika eneo la Bugabo Bukoba vijijini, na mwaka 2006 walichuja aina 201 ambazo walichambua na kupata aina nane tu 2008 na hatimaye 2011 zikapatikana aina nne zenye ubora, huyu ni Dr. Mariatabu Ng’oma kutoka kituo cha utafiti Maruku mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa sera ya kilimo nchini, halmashauri zote zinapaswa kutenga asilimia 20 ya pato la kahawa kila mwaka kwa ajili ya kuwezesha wakulima katika upatikanaji wa pembejeo, Dr. Mariatabu anasema ni halmashauri ya Bukoba pekee yenye kasi kubwa katika kuwapatia wakulima wake miche elekezi ya kahawa, mpaka sasa imeshasambaza miche elfu 65 na 391 kwa lengo la kufikisha miche laki tatu bure kwa wakulima ifikapo mwezi October mwaka huu 2017.

Sautiyamnyonge imetembelea kitaru cha Ibwera Bukoba vijijini, kilomita 59 kutoka Bukoba mjini, ambacho kilianzishwa mwaka 1996, kina uwezo wa kuzalisha miche laki moja kwa mwaka na tangu januari hadi mei mwaka huu tayari kimezalisha miche elfu 40.

Uzalishaji wa kahawa katika halmashauri ya Bukoba kwa msimu, ni kati ya elfu 3 na 500 hadi elfu 4, msimu unapokuwa mzuri kulingana na mabadiliko ya tabianchi, kutoka mashamba ya wakulima elfu 3 na 751 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2012.

Ili kujua kwanini halmashauri hiyo imeamua kuweka nguvu katika zao la kahawa kwa kipindi cha miaka mitano, mwandishi wa sautiyamnyonge amefanya mahojiano na Geofrey Luvumbagu, ambaye ni afisa mfuatiliaji wa maendeleo ya kahawa halmashauri ya Bukoba.

AFISA KILIMO

Kitongoji Kajumilo kipo kijijini Kikomero halmashauri ya Bukoba, na sautiyamnyonge imefika katika eneo la Kyante anapopatikana mkulima na mshindi wa uzalishaji kahawa kitaifa mwaka 2016, akihudumia shamba la hekari 32 ambazo humuwezesha kuvuna kati ya tani 10 na 15 kwa msimu mmoja, wapo wengi waliokata tama ya kuendeleza zao la kahawa, lakini ni tofauti kabisa na Thomas Marco.

Igawa kahawa inalimwa kwenye halmashauri nane za mkoa wa Kagera, inasimamiwa na halmashauri husika kupitia bajeti zinazotengwa kwenye vikao vyake kwa kushirikisha wadau wa kilimo hicho kama vyama vya ushirika, makampuni ya ununuzi, na bodi ya kahawa mkoa, ingawa idara zote hizo ziko chini ya afisa kilimo mkoani Kagera Godwin Vedastus,  tumetaka kujua wajibu wa mkoa katika kuendeleza zao la kahawa ni nini?

Kuwezesha uzalishaji wa kahawa kufikia malengo ya mkoa kunawezekana na hatimaye kurudisha mkoa katika nafasi yake kiuchumi nchini, lakini lazima matumizi ya pembejeo zinazokinzana na magonjwa, matumizi sahihi ya mbolea na kuzingatia maelekezo ya maofisa ugani yazingatiwe.

Wakulima wa kahawa mkoani Kagera, wanajivunia kuwa na udongo unaopata mvua za mara kwa mara, ingawa taalamu wanasema kuwa mvuas hizo huondosha kiasi kikubwa cha mbolea ya asili, samadi hivyo kushauri kuwa wakitumia mbengu kizani kwa magonjwa sambamba na mbolea ya viwandani, uzalishaji wa sasa utaongezeka mara mbili .

Mwandishi wa sautiyamnyonge amefanya mazungumzo  na Dr. Mariatabu Ng’omba kutoka TACRI pamoja na Almas mtaalamu wa mbolea kutoka kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo Maruku mkoani Kagera.

Wameelekeza wakulima watumie mbolea ya madukani na kuwasiliana na TACRI Maruku kwa lengo la kupata uashauri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close