AfyaKilimo

LUMBESA: makuli Mtwara walalamikia ujira mdogo kwa madhara makubwa kiafya

Wakati baadhi ya wafanyabiashara wakianza kununua mazao mapya kwa wakulima wa mazao ya nafaka, wachukuzi wa mizigo wamewaomba wafanyabiashara hao kuzingatia vipimo sahihi vya ujazaji wa mzigo katika gunia ili kulinda afya za wabebaji pamoja na maslahi ya malipo yao. 
 
Wakizungumza na Sauti ya Mnyonge mkoani Mtwara wachukuzi hao wamedai kuwa ushindiliaji na ushonaji wa magunia kama kichuguu maarufu kama lumbesa umekuwa ukiwaumiza huku malipo ya shilingi 500 wanayolipwa, ambayo ni bei ya kushusha na kupakia gunia la kilo mia moja, ikiwaumiza.


 
Kwa upande wao wafanyabiashara wamedai kuwa wanalipa kiasi hicho cha fedha kwa wachukuzi kutokana na bei iliyopangwa na serikali huku sababu za kujaza rumbea wakieleza kuwa ni kutokana na ushuru wa mageti kila kijiji.
 
Bi Rukia Salum, ambaye alikutana na mwandishi wa Sauti ya Mnyonge, alikuwa na haya ya kusema kama alivyonaswa na kamera ya Sauti ya Mnyonge:

Mfanyibiashara mwingine wa mjini Mtwara, Athuman Nampamba, naye aliongea na Sauti ya Mnyonge na kueleza yake kuhusiana na biashara hiyo akisema:

Je, ni nini maoni yako kuhusu aina hii ya ufungaji wa bidhaa za mazao toka kwa wanyonge? 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close