Kanda ya KusiniMtwara

Madiwani mkoani Mtwara wapigwa msasa kuhusu taratibu za kiutendaji

KUTOKANA na udhaifu mkubwa uliopo katika kufanya maamuzi mbalimbali kwa madiwani  nchini serikali imetoa elimu itakayowawezesha kujua Kanuni, Sheria na Taratibu za utumishi wa umma.

Akizungumza katika mafunzo hayo ya madiwani wa mkoa wa mtwara yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ufadhiri USAID na kuendeshwa na chuo cha serikali za mitaa Homboro.

Mwakilishi wa chuo cha serikali za mitaa Hombolo Dr Henry Jonathan amesema kuwa mafunzo hayo ya uimarishaji wa mfumo ya huduma za umma na utawala bora (PF3) yameletwa ili kuwawezesha madiwani kutoa maamuzi sahihi.

Alisema kuwa Madiwani wengi nchini wamekuwa na tatizo la kutoelewa kanuni jambo ambalo limekuwa likipelekea maamuzi yao kuwa na udhaifu kutokana na kutofuata kanuni, sheria na taratibu za uendeshaji wa halmashauri zetu.

Jonathan alisema kuwa kutokana na kutambua hilo serikali imeona vema kuendesha mafunzo hayo kwa watoa maamuzi katika Halmashauri zetu ili waelewe Sheria, Kanuni na Taratibu katika kufanya maamuzi ili kuruhusu mifumo iweze kufanyakazi vizuri.

“Unajua wapo madiwani wapya na hawajui kanuni, sheria na taratibu za uendeshaji wa halmashauri ndio maana serikail imelazimika kutoa elimu kwao ili waweze kufanya maamuzi sahihi”

Zipo kanuni zinazowaruhusu wakuu wa wilaya kutoa ushauri kwa madiwani hasa pale wanapoona kuwa kuna maamuzi yasiyo sahihi yanayokuwepo na ukiukwaji wa sheria na taratibu” alisema Jonathan

Akizungumzia mradi huo Meneja wa Mradi wa uimarishaji wa mfumo ya huduma za umma na utawala bora (PF3) Mkoa wa Mtwara Deusdedit Msofe anasema kuwa mafunzo hayo  yanalenga kuwapa uwezo wa kusimamia fedha zinazotengwa kwenye miradi ya Halmashauri.

Alisema kuwa lengo ni kuhakisha kuwa wanajua majukumu yao vizuri ili wawezi kusimia vizuri fedha zinazotengwa na Halmashauri na serikali kuu na zile zinazotengwa halmashauri ili miradi iweze kutelekezwa kwa ufanisi zaidi.

“Katika mafunzo haya tunaamini kuwa wataongeza uwezo wao wa kuhoji mambo mbalimbali yakatika vyanzo vya mapato, usimamizi na uibuaji wa miradi ya katika kusimamia serikali za halmashauri vizuri kwa upande wa halmashauri na kudhibiti na kubainisha majukumu yao vizuri” alisema Msofe

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close