Kanda ya KusiniKilimo

Mkurugenzi awakingia kifua wakulima wa choroko wilayani Nanyumbu

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara Hamisi Dambaya ameonya wafanyabiashara wa zao la choroko kuacha tabia ya kuwalaghai wanyonge kwakutumia vifaa haramu kupimia zao hilo.

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kukamata wafanyabiashara watatu wakiwa na mizani ambayo haijahakikiwa na wakala wa vipimo alisema kuwa walanguzi hao wamekuwa wakitumia mizani fake kuwaibia wakulima.

Ambapo alisema kuwa  vifaa  hivyo haramu ndio vimekuwa vikitumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa wakulima wa zao hilo ambao wamekuwa wakidhurumiwa na kukoseshwa haki yao kutokana na udadanyanyifu wanaotumia wafanyabiashara wa zao hilo la choroko.

“Serikali haitavumilia huu ulanguzi  ndio maana tuna sisitiza vita dhidi ya ulanguzi unaofanywa na wafanyabiashara hawa mizani haijadhibitishwa wanatumia kwa kificho lazima hii iwe vita kwa wakulima wenyewe, vyama vya ushirika sio ya serikali pekee lazima tushirikiane ili kuimaliza hatuko tayari kuendelea kuona mkulima akidhurumiwa……….

“Sisi hatuwezi kukaa kimya tukiendeleea kuona mkulima akinyonywa na akiendelea kudhurumiwa na wafanyabishara wachache ambao pamoja na dhuruma wanaikosesha halmashauri mapato mengi ambayo yangeweza kuongeza huduma za jamii zikiwemo barabara, maji na shule” alisema Damumbaya

“Hili zoezi zima linaendeshwa kisheria ndio maana tunafuata sheria zote za usalama wa chakula ya mwaka 2012 ambayo imetoa mwongozo na namtaka mnunuzi kununua kwenye maghala na wasinunue nje ya muda……. 

“Hivi sasa  wakulima wa zao la Choroko wanauza kwa bei ya shilingi mia saba mpaka mia tisa wakati  bei dira iliyopangwa na serikali kilo moja inatakiwa kuuzwa kwa bei  ya shilingi  elfu moja na mia mbili” Alisema Damumbaya

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima wa zao hilo walioongea na Sauti ya Mnyonge, wameiomba serikali kusaidia katika utafutaji wa masoko ya zao lao ili waweze kunufaika na kilimo hicho, kwani wanakitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku. 

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close