ElimuKanda ya Kusini

Uhaba wa madarasa waendelea kuitesa shule ya msingi Michenji

Wanafunzi wa shule ya msingi Michenji iliyoko katika kata ya Nanguruwe wilayani Mtwara wanalazimika kusomea chini ya miti kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa
 
Wanafunzi hao wameiomba serikali kuweka jitihada za ujenzi wa madarasa kama ilivyofanya kwenye utengenezaji wa madawati ambayo wameyapanga chini ya miti nan a kwenye vibanda vya nyasi. 

 
Akizungumza ,Saidi Abdullahman ni mwenyekiti wa kijiji cha Nanguruwe ilipo shule hiyo anasema kuwa wao kama wanakijiji wameanza kufyatua ambapo wanaomba serikali iwasaidie kukamilisha ujumbe. 

 
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Omary Kipanga amesema kuwa serikali ipo katika mkakati wa kutatua changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa kupitia kampeni ya ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa huo Halima Dendego kampeni ya Benki ya Matofali. 

 
Shule ya Msingi Michenji yenye darasa la awali hadi la saba ina jumla ya wanafunzi 371 huku darasa la awali,la tatu na la sita wakisomea chini ya miti na walimu nao ofisi zao zikiwa chini ya miti.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close