AfyaKanda ya Kusini

Kinamama washiriki na kufurahia ujenzi wa zahanati kata ya Lukuledi

Akinamama katika kata ya Lukuledi, wamepaza sauti zao wakiwataka wananchi katika kata hiyo na jimbo la Ndanda kwa ujumla, kuweka kando tofauti zao za kisiasa, ili kuweza kujiletea maendeleo kwakuwa maendeleo hayachagui itikadi za kisiasa bali humnufaisha kila mtu. 

Akina mama hao wamepaza sauti zao walipoongea na Sauti ya Mnyonge, iliyowatembelea walipokuwa wakishiriki katika mradi wa ujenzi wa zahanati ya kata hiyo, zahanati ambayo inatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa kata hiyo ambao walikuwa wakilazimika kwenda mbali kupata huduma za afya. 

Mbali ya kwenda mwendo mrefu kupata huduma hizo, wakazi hao walikuwa wakilazimika pia kushiriki shughuli za usafi kabla ya kupata huduma za matibabu katika hospitali ya Chikunja walikokuwa wakilazimika kwenda kupata huduma hizo za matibabu.


Mwananchi akieleza adha waliyokuwa wakiipata ya kufanyishwa usafi walipoenda kupata matibabu zahanati ya serikali

Mbunge wa jimbo la Ndanda Cecil Mwambe (CHADEMA) ambaye alishiriki katika tukio hilo, alieleza kusikitishwa na taarifa za wananchi wa kata hiyo ya Lukuredi kufanyishwa usafi katika zahanati za serikali wakati wanapoenda kupatiwa huduma ya afya.

Akizungumza wakati wa ujenzi wa msingi wa zahanati ya kijiji cha Lukuredi A alisema kuwa amelazimika kuwapunguzia adha ya upatikanaji wa huduma za afya wakazi wa kata hiyo  kutokana na wakazi hao kutembea umbali mrefu huku wakilazimishwa kufanya usafi ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

Alisema kuwa kitendo hicho kimekuwa kikivumiliwa na wakazi wa kata hiyo kutokana na kutokuwa na njia mbadala ya kupata huduma hiyo mbali na uwepo wa zahanati ya kidini ambayo hulazimika kutumia gharama kubwa ili kupata matibabu.

“Ninafahamu kuwa kata hii na Jimbo la Ndanda kwa ujumla kuna changamoto nyingi katika elimu, miundombinu, maji na nyingine nyingi lakiini tumeweka kiupembele kwenye huduma ya afya katika kata hii kwakuwa lilikuwa ni tatizo kubwa linalowasumbua wakazi wa kata hii na vijiji vya jirani….

“Huu ni mwanzo tu wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu ikiwemo kujitolea ili kuweza kutimiza adhama na malengo yaliyokusudiwa wale watakao kiuyuka basi sheria za kijiji zipo zitumike ili kuweza kubana kwa mujibu wa sheria najua tupo hapa na Diwani na Mwenyekiti wa kijiji hicho” alisema Mwambe


Mwananchi akieleza kusikitishwa na wananchi wenzake kutoshiriki ujenzi wa zahanati

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close