Uncategorized

Wanawake wanyonge wanusuru wanyonge na watoto wao kwa mbadala wa maziwa.

Ushirika ulioundwa na akina mama maskini mwaka 2016 katika wilaya ya Bukoba ukiwa na vikundi vitatu, umeweza kuibuka na mbinu mpya inayoweza kuwa mbadala wa maziwa pamoja na lishe kwa lengo la kupunguza au kuondoa kabisa utapiamlo mkoani Kagera.

Kutokana na hali hiyo, wananchi mkoani Kagera, wameshauriwa kutumia fursa ya kulima zao la soya, ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa za urutubishaji jamii na kupunguza hali ya hudumavu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Mwenyekiti shirika la Bukoba women empowerment association -BUWEA, Bi Regina Majaliwa , amesema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa sautiyamnyonge, kwamba shirika hilo linanunua soya kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wa kutoka nje ya Kagera, baada ya kiasi kinachozalishwa na wanachama wake kuwa kidogo.

Amesema kuwa zao hilo limekuwa na matumizi mengi na muhimu baada ya kulisindika kwa kupata maziwa ya chai, yaliyogandihswa kwenye pakti kwa kuuza bei ya chini ya shilingi 300 hadi 800 kwa lita, na unga kwa matumizi majumbani na hasa kusaidia watoto kukua na afya njema na kupunguza udumavu mkoani Kagera.

Mwandishi wa sautiyamnyonge ametembelea ofisi za BUWEA na kuandaa makala fupi.

Taarifa za ushirika huo, zinasema kuwa wanashindwa kupata kiasi cha kutosha cha soya ili waweze kusindika maziwa ya kutosha, ambavyo mpaka sasa wananunua kwa wanachama wao ambao wanashindwa kuzalisha vya kutosha, kutokana na zao hilo kustawi zaidi wilayani Karagwe.

Kilo moja ya soya inanunuliwa na BUWEA kati ya shilingi elfu moja na 300 hadi 400, hivyo jamii ikijikita zaidi kulima zao hilo, itaweza kujiingizia kipato na kunusuru afya ya jamii baada ya maziwa ya ng’ombe na mbuzi kuwa adimu au kupatikana kwa bei ya juu ya shilingi kati ya elfu moja na 200 hadi 500 kwa lita.

Bi Jesca Jonathan, ameueleza mtandao huu kuwa wao huzunguka kuhamasisha wakina mama kujiunga, kwa lengi la kuhakikisha wanaikwamua jamii hasa kutambua matumizi ya vyakula vitokanavyo na soya ili kupata mbadala wa maziwa ambayo ni adimu kwa mkoa wa Kagera.

Bukoba women empowerment association -BUWEA , ilianzishwa mwaka 2016 ikiwa na wanachama 30 kupitia vikundi vitatu, na sasa inavyo vikundi 82,vyenye wanachama 820 kutoka manispaa na halmashauri ya Bukoba, ili kuwawezesha akina mama katika kukuza maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close