Elimu

Ujenzi ofisi za walimu Dar kuanza rasmi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda* leo amezindua rasmi zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa *Ofisi za kisasa 402 za Walimu* ambapo amewasihi Wadau na Wananchi kuunga Mkono jitiada hizo.

Katika uzinduzi huo  *RC Makonda* ameshiriki zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya Ujenzi huo.

*Makonda* amesema lengo la Ujenzi wa Ofisi hizo ni *kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu* ili waweze kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.

*Amesema* wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.

*RC Makonda* ametoa wito kwa Wananchi na Wadau *kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi* ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.

Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu  wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea *kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.*

Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata *mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji* Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.

*Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo* kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au *Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.*

*Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori* na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

Katika hatua nyingine *RC Makonda* amesema *atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko* ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za *Rais DR.JOHN MAGUFULI* ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.

Kwa upande wake *Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kanali Charles Mbuge* amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya *Million 200* ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close